HabariPilipili Fm

Mke Wa Marehemu Rogo Akamatwa.

Maafisa wa kupambana na ugaidi ATPU wamemtia mbaroni mjane wa marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye aliuawa miaka 4 iliyopita nyumbani mwake eneo la kikambala kaunti ya kilifi.

Haniya Said Saggar alikamatwa baada ya maafisa kadha wa kikosi cha kukabiliana na ugaidi kuvamia nyumba yake siku ya jumatano jioni.

Inaarifiwa maafisa hao walichukua simu yake ya mkono kabla ya kumuingiza ndani ya gari na kumsafirisha katika eneo lisilojulikana.

Kulingana na jamaa wa familia, maafisa wa polisi walidai kumpeleka katika kituo cha polisi cha mtwapa, ila baada ya kutembelea kituo hicho badae hawakumpata.

Show More

Related Articles