HabariMilele FmSwahili

Makau Mutua:Nitaheshimu na kushirikiana na uongozi wa rais Uhuru Kenyatta

Profesa wa sheria Makau Mutua anasema ataheshimu na kushirikiana na uongozi wa rais Uhuru Kenyatta iwapo atachaguliwa kama jaji mkuu.Akijibu swali kuhusiana na ujumbe alioweka kwenye mtandao wake wa twitter kuhusu kutomtambua rais Kenyatta, Mutua amejitetea akisema msimamo huo ulikuwa wa kibinafsi akihusisha ujumbe wake na kesi zilizokuwa mahakamani ICC wakati huo.
Makau ameiambia tume ya JSC yuko radhi kuasi uraia wake wa Marekani iwapo ataidhinishwa kama jaji mkuu.
Na kuhusu haki za wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini,Mutua anasema kila mkenya anafaa kulindwa kisheria na kuwa kila mtu yuko huru kuishi anavyotaka.

Show More

Related Articles