HabariMilele FmSwahili

Wazee wa jamii ya Kipsigis wataka wabunge Charles Keter na Joseph Limo kuomba msamaha

Baraza la wazee wa jamii ya Kipsigis limewasuta waziri Charles Keter na mbunge wa Kipkelion mashariki Joseph Limo kwa kuidhinisha ujenzi wa bwawa la Itare. Baraza hilo linadai wawili hao wamekiuka matakwa ya jamii hiyo kwa kuruhusu mradi huo bila mashauriano.Wazee hao wametishia kutounga mkono serikali ya Jubilee iwapo viongozi hao hawataomba msamaha. Hata hivyo, wenyeji wa Rongai na Kuresoi wamewakosoa wazee hao kwa kuingiza siasa katika mradi huo na kuitaka serikali kutobabaishwa na vitisho vyao.

Show More

Related Articles