HabariMilele FmSwahili

Wenyeji wa Bomet wakubwa na uhaba wa maji

Wenyeji katika kaunti ya Bomet wanaishi kwa hofu wa kupata maradhi yanayortokana na uchafu kufuatia uhaba wa maji uliokumba kaunti kwa muda wa wiki moja. Inadaiwa uhaba huo umetokana na kukatizwa kwa nguvu za umeme katika mtambo wa kupiga maji kwenye mto wa kipsonoi. Wenyeji wamelalamikia hali hiyo na kuitaka idara husika kuchukuwa hatua za dharura .Afisa mkuu wa kampuni ya kusambaza maji mjini humo (BOWASCO) David Cheruiyot amewataka kuwa na subira swala hilo likitatuliwa.

Show More

Related Articles