HabariPilipili Fm

Wakaazi Wa Kilifi Wagizwa Kushirikiana Kukabiliana Na Uhalifu

Kamishna wa kaunti ya Kilifi Joseph Keter amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kushirikiana pamoja na kamati za nyumba kumi ili kukabiliana na wahalifu.

Katika kikao na waandishi wa habari Keter amesema wananchi  wenyewe ndio wanaweza kutoa habari za kijasusi kwa maafisa wa polisi kuhusu visa vya uhalifu.

Keter amebaini kuwa eneo la Watamu limekuwa likikumbwa na visa vingi vya uhalifu, na hivyo kutoa changamoto kwa kamati za nyumba 10 kutoa ripoti zao kwa vyombo vya usalama kila wakati.

Show More

Related Articles