HabariK24 TvSwahiliSwahili Videos

Gavana Gachagua amefika Seneti na kumshtumu mwanasiasa Ephraim Maina

Gavana wa kaunti ya Nyeri Nderitu Gachagua ameliambia bunge la Senate kwamba mpinzani wake mkuu, aliyekuwa wakati mmoja mbunge wa mathira Ephraim Maina ndiye anayepanga njama ya kutaka aondolewe afisini.
Akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha uchunguzi wa madai anayolimbikiziwa, Gachagua pia amefichua kuwa waakilishi wa kaunti ya Nyeri walikuwa na njama ya kutaka wapokezwe hongo ya shilingi milioni sita kila mmoja na alipodinda wakaanza kumpiga vita.
Anders Ihachi ana taarifa hiyo ambapo Gachagua sasa ni gavana wa tatu kukodolewa na zimwi hili baada ya Martin Wambora wa Embu na Paul Chepkwony wa Kericho walioponea mjeledi wa senate.

Show More

Related Articles