HabariMilele FmSwahili

Watu elfu 18 hufariki kila mwaka kwa ugonjwa wa saratani

Serikali inaendelea na mpango wa kuhakikisha kila kaunti ina kituo cha kukabili ugonjwa wa saratani. Waziri wa afya Dr Cleopa Mailu anasema watu elfu 18 hufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huo hali anayosema inahitaji hatua za dharura.Akizungumza katika kongamano la afya lililoandaliwa mapema leo katika ikulu ya rais, Mailu amesema serikali imewekeza mabilioni ya fedha kuhakikisha hakuna mgonjwa anayeondoka nje ya taifa kutafuta matibabu ya saratani.

Show More

Related Articles