HabariMilele FmSwahili

Githu Muigai ampatia Ann Amadi wakati mgumu

Mwanamume mmoja amewasilisha ombi mbele ya tume ya huduma za mahakama akitaka kuondolewa afisini msajli mkuu wa mahakama Ann Amadi.Anadai Amadi hafai kusalia afisini kwa kudhihirisha mapendeleo katika kesi inayomkabili jaji mmoja.Haya yanajiri wakati tume hiyo ikiendelea kuwahoji waliotuma maombi ya kuhudumu kama jaji mkuu.Aliyefika mbele ya tume hiyo leo ni wakili Lucy Wanja.Wanja ambaye ni mwanamke wa pili kuhojiwa alikabiliwa na wakati mgumu baada ya mwanasheria mkuu Githu Muigai kumtaka aeleze ni kwanini tume ya elimu ya vyuo vikuu nchini anakohudumu kama kamishana imekosa kuvichukulia baadhi ya vyuo vikuu hatua licha ya kutoa elimu ya uanasheria bila kuidhinishwa.

Show More

Related Articles