HabariPilipili Fm

Achani Ataka Wanaofuja Pesa Za Kina Mama Kuadhibiwa.

Naibu gavana kaunti ya Kwale Fatuma Achani ameitaka idara inayosimamia maswala ya maendeleo ya jamii, michezo na jinsia katika kaunti hiyo kuchunguza visa  vya makundi ya kinamama ya kuwekeza  vijijini ambayo yamekuwa  yakidhulumiwa fedha zao na walimu  wao.

Haya ni baada ya makundi 6   yenye wanachama 35 kila kundi eneo la Dzombo, kulalamikia kulaghaiwa zaidi ya shilingi laki mbili.

Achani amewataka maafisa wa idara hiyo kuchukua hatua za haraka kuwasaka  wahusika na kuwachukulia hatua kali za kisheria, huku akiitaja hatua hiyo kama yenye kuzorotesha maendeleo ya kina mama katika kaunti hiyo.

Show More

Related Articles