HabariMilele FmSwahili

Kasisi anazuiliwa Ruiru kwa madai ya kuwaibia wanafunzi vipakatalishi

Polisi huko Ruiru wanamzuilia kasisi anayedaiwa kuwaibia vipakatalishi wanafunzi kadhaa kutoka vyuo vikuu vya Kenyatta, Jomo Kenyatta, Zetech na chuo cha Nairobi Institute of Business Studies. Mkuu wa polisi eneo hilo Isaac Thuranira anasema jamaa huyu kwa jina kasisi Stephen Ochieng alinaswa akiwa na vipakatalishi vitano baada ya kuwahadaa wanafunzi hao kuwa angewasaidia kupata ajira. Inaarifiwa kuwa amekuwa akiahidi kuwatafutia ajira katika shirika moja la kanisa na kuwataka kuhudhuria mahojiano wakiwa na vipakatalishi vyao

Show More

Related Articles