HabariMilele FmSwahili

Rais Uhuru azungumza na rais wa Tanzania Pombe Maghufuli

Rais Uhuru Kenyatta leo amefanya mazungumzo ya simu na rais wa Tanzania John Pombe Maghufuli na waziri mkuu wa Uingereza Therisa Mei na kukubaliana maswala kadhaa.Akizungumza na Mei Uhuru wamekubaliana kuimarisha ushirikiana kukabili ugaidi, ufisadi, sawa na kuimarisha biashara na uwekezaji.Katika mazungumzo waliofanya kwa njia ya simu, Uhuru amempongeza Mei kwa uteuzi wake kama waziri mkuu wa Uingereza
Akizungumza na maghufuli, uhuru ametuma risala zake za rambi rambi kwa familia za tetemeko la jana mkoa wa Bokoba nchini Tanzania. Ameagiza wanajeshi wa KDF kusafirisha mabati 4000, blanketi 400 na magondoro 100 kuwasaidia waathiriwa wao.Zaidi ya watu 16 wamefariki na wengini 200 kujeruhiwa katika tetemeko la jana katika eneo la Bukoba nchini Tanzania

Show More

Related Articles