HabariMilele FmSwahili

Rais Uhuru kuhudhuria kongamano la kujadili juhudi za kukabiliana na ukimwi

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria kongamano la tano kuhusu juhudi za kukabiliana na ukimwi, malaria na kifua kikuu litakaloandaliwa Motreal Canada. Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu Manioah Esipisu rais ambaye amepokea mwaliko wa waziri mkuu wa Canada Justin Tredeau atazungumzia manufaa ambayo Kenya imepata katika kukabiliana na magonjwa hayo kwa miaka mitatu iliyopita. Kutoka Canada rais ataelekea New York Marekani ambako atahudhuria kikao cha 71 cha baraza kuu la umoja wa mataifa. Kikao hiki kinatarajiwa kujadili maswala ya wakimbizi na hatua ya Kenya kufunga kambi ya Daadab. Rais pia ameratibiwa kuhutubu katika kongamno la kibiashara baina ya Marekani na Afrika.

Show More

Related Articles