HabariMilele FmSwahili

Raia wafurahia ajali iliyotokea kwenye barabara ya Primarosa Mombasa

Kumekuwa na kihoja katika eneo la Primarosa bara bara ya Mombasa wakati wakaazi wameamua kujinyakulia mahindi ya bwerere wakati lori lililokuwa likisafirisha mahindi hayo kuhusika kwenye ajali. Lori hilo lililokuwa safarini kutoka Mombasa kuja hapa Nairobi lilibingirika baada ya kukwepa kugongana na gari lingine. Juhudi za polisi wa trafiki kuzuia mamia ya wenyeji hao kuiba mahindi zimefeli huku shughuli za uchukuzi zikitatizwa kwa muda kwenye bara bara hiyo.

Show More

Related Articles