HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi wa shule ya Netima Kaunti ya Bungoma wafanya maandamano

Wanafunzi wa shule ya wavulana ya upili ya Netima kaunti ya Bungoma wameafanya maandamano leo kulalamikia baadhi ya maagizo kutoka mwalimu mkuu wao ili kuruhusiwa kuendelea na masomo. Hata hivyo juhudi zao za kutaka kuwasilisha malalamishi katika afisi za elimu eneo la Bumula zimeambulia patupu kwani hakukuwa na maafisa ofisini leo ikiwa siku kuu ya kitaifa. Mwalimu mkuu Wyclif Namianya anasema wanafunzi hao waliwahadaa walinzi wa shule hiyo mapema hii leo kuwa wanaelekea katika mazoezi ya kukimbia kabla ya badala yake kuandamana.

Show More

Related Articles