HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya magari 10 yanayoshukiwa kuibwa yanashwa Kitengela

Zaidi ya magari 10 yanayoshukiwa kuibwa yamepatikana katika eneo moja mtaani Newvalley huko Kitengela. Magari hayo yakiwemo malori matatu ambayo hayakuwa na nambari za usajili yamepatikana na askari wa kaunti ya Kajiado waliofika eneo hilo kukagua shughuli ya ujenzi. Washukiwa kadhaa waliokuwa katika eneo hilo wamefanikiwa kutoweka. Msimamizi wa wadi ya Kitengela Moses Kamalik, amesema mmiliki wa eneo hili hajatambulika. Inspekta mkuu wa Kitengela Moses Tirike amesema uchunguzi umeanzishwa kuwakamata wahusika na kubaini yalipotoka magari hayo.

Show More

Related Articles