HabariMilele FmSwahili

Waislamu wanadhimisha siku kuu ya Eid Ul Adha loe

Waumini wa dini ya kiislamu leo wanaungana katika maeneo mbali mbali nchini kuadhimisha siku kuu ya Eid Ul Adha. Mjini Mombasa waumini wanajumuika katika uwanja wa Ronadl Ngala huku swala ya siku kuu inaongozwa na kadhi mkuu nchini. Hali kama hiyo inasahuhudiwa katika kaunti ya Isiolo ambapo waumini wanajumuika katika uwanja wa Isolo katika sherehe itakayoongozwa na imam mkuu kaunti hiyo Abdulaziz Yusuf ambapo maswala mbali mbali ikiwemo mzozo baina ya jamii ya wafugaji yatajadiliwa. Baada ya swala waislamu watasherehekea kwa kuchinja mbuzi na kondoo alivyofanya Ibrahim kama ishara ya kujitolea kumtumikia mwenyezi mungu

Show More

Related Articles