HabariMilele FmSwahili

Kero la virusi vya HIV na matumizi ya dawa za kulevya lajadiliwa

Serikali za kaunti zimetakiwa kubuni kanuni maalum ili kufanikisha huduma za afya kwa kila mwananchi hasa watu ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya na virusi vya HIV.akiongea kwenye warsha iliyoandaliwa na shirika la REACHOUT  kuhamasisha  wananchi kuhusu athari za dawa za kulevya, aliyekuwa kamishna wa tume ya utekelezaji wa katiba Catherene Muma, amesema kulingana na katiba huduma za afya zimegatuliwa na hivyo ni jukumu la serikali za kaunti kuweka mikakati na sera dhabiti ili kuboresha huduma za afya katika kaunti zao.Naye mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir aliyehudhuria hafla hiyo alilaumu polisi kwa kuwakamata vijana kiholela kwa  madai ya matumizi ya dawa za kulevya.

Show More

Related Articles