HabariK24 TvSwahiliSwahili Videos

Jubilee na ODM kudhihirisha ubabe kesho Nairobi na Mombasa

Kiongozi wa ODM na mmoja wa vinara wa muungano wa CORD Raila Odinga tayari ametua katika jiji la Pwani Mombasa tayari kwa mkutano mkuu wa kuadhimisha miaka kumi ya chama cha chungwa, ODM.

Huku Nairobi ugani Kasarani maandalizi ya wakati kiongozi wa chama kipya cha Jubilee party rais Uhuru Kenyatta anafaa kuhutubia taifa yamekamilika.

Anders Ihachi anatathmini ubabe huu wa kisiasa ambao unatarajiwa kushuhudiwa kati ya chama kipya cha Jubilee na chama kilichobuniwa miaka 10 iliyopita cha ODM kwenye mwamko wa siasa za uchaguzi wa mwaka 2017.

Show More

Related Articles