MichezoPilipili Fm

Real Madrid Na Atletico Madrid Zimepoteza Rufaa Zao.

Real Madrid na Atletico Madrid zimepoteza Rufaa zao dhidi ya Adhabu za FIFA na sasa zimepigwa marufuku kusajili Wachezaji Wapya katika Madirisha ya Uhamisho Mawili yajayo.

Awali Klabu hizo 2 za Jijini Madrid Nchini Spain zilipatikana na hatia na FIFA kwa kukiuka Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji wa Chini ya Umri wa Miaka 18.

Hii Leo FIFA imetoa Taarifa kuthibitisha kuwa Rufaa za Real na Atletico zimetupwa na sasa watatumikia Adhabu ya kutoruhusiwa kusaini Wachezaji Wapya katika Madirisha ya Uhamisho Mawili yajayo.

Hilo linamaanisha, Klabu hizo hazitaweza kusaini Mchezaji Mpya katika Dirisha la Uhamisho la Januari 2017 na lile la kuanzia Julai hadi Agosti 2017 na kuwa Huru kusaini wapya kuanzia Januari 2018.

Mbali ya Kifungo hicho cha Kusaini Wachezaji Wapya, Real na Atletico pia zimetwangwa Faini za Pauni 622,000 kwa Atletico na Pauni 249,000 kwa Real.

Klabu hizo pia zimepewa Onyo kali pamoja na Siku 90 za kurekebisha kasoro zote za Wachezaji waliowatia hatiani.

Hata hivyo, kufungiwa Kusaini Wachezaji Wapya hakumaanishi hawewezi kununua Wachezaji Wapya kwani hilo ni ruksa ila Wachezaji hao Wapya hawatasajiliwa na hawataruhusiwa kucheza hadi Adhabu yao imalizike.

Hali hii iliwahi kuwakuta Barcelona ambao walimnunua Arda Turan lakini alikuwa haruhusiwi kucheza hadi Adhabu ya Barca ilipoisha.

 

Show More

Related Articles