HabariMilele FmSwahili

Mshukiwa wa ubakaji ajaribu kujiua Kotini Nakuru

Mvulana wa miaka 19 na ambaye ameshtakiwa na kosa la ubakaji ameshangaza mahakama ya Nakuru leo baada ya kujaribu kujitoa uhai kwa kunywa kemikali.Hezbon Koskei alikuwa ameshtakiwa kwa kumbaka mtoto katika eneo la Njoro madai ambayo alikanusha.Mshtakiwa alikuwa amebeba chupa ambayo ilidhaniwa kuwa ni ya maji na alipofikishwa kotini alianza kunywa kabla ya kuzirai na kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa bonde la ufa iliyoko Nakuru.Anaendelea kutibiwa kesi yake ikitarajiwa kuendelea punde tu atakapo pata nafuu

Show More

Related Articles