HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 3 wa ujambazi wauwawa katika visa tofauti hapa jijini Nairobi

Washukiwa watatu wa ujambazi wameuwawa katika visa viwili tofauti hapa jijini Nairobi. Wawili kati yao walipewa kichapo na umma hadi kufa baada ya jaribio lao la ujambazi mtaani Buru Buru kutibuka. Polisi wanasema jamaa hao wenye miaka 22 na 24 waliingia katika nyumba moja mtaani humo na kumdunga kisu kijana mwenye umri wa miaka 18 kabla ya kukabiliwa mshukiwa wa tatu ameuwawa kwa kupigwa risasi mtaani Isilii huku mwenzake akifanikiwa kutoroka. bastola moja na risasi nne zilinaswa

Show More

Related Articles