HabariMilele FmSwahili

William Okedi afikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya ofisi

Afisa mkuu mtendaji wa NACADA William Okedi amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya afisi.Okedi anashtakiwa kwa kukosa kutafutia NACADA washauri kusimamia hazina ya kudhibiti matumizi ya pombe nchini kama alivyotakiwa.Ameshtakiwa kwa kutoa kandarasi ya milioni 12.8 iliyopewa kampuni ya ERMNST and YOUTH ambayo inasimamia hazina hiyo kinyume na sheria.Hata hivyo Okedi amekanusha mashtaka hayo.

Show More

Related Articles