HabariMilele FmSwahili

Bi Kenyatta amechangisha millioni 12 kuwasaidia watoto wenye maradhi ya moyo

Mkewe rais Margeret Kenyatta amechangisha milioni 12 za kuwasaidia watoto wenye maradhi ya moyo kufanyiwa upasuaji nchini Israel. Fedha hizo zimechangishwa katika hafla iliyoandaliwa na shirika la Save a Child Heart Kenya. Bi Kenyatta amepongeza mchango wa shirika hilo nchini na mpango wake kuwafaa watotp 100 wenye matatizo ya moyo katika miaka kadhaa ijayo. Fedha zilizochangishwa zitafadhili gharama ya usafiri na malazi kwa watakaonufaika.

Show More

Related Articles