HabariPilipili Fm

Shughuli Za Usafiri Kuimarika Malindi.

Shughuli za usafiri mjini Malindi huenda zikaimarika kufuatia mpango wa Serikali ya kaunti ya Kilifi wa kuzindua barabara kadhaa mjini humo.

Gavana wa Kilifi Amason Kingi amesema hatua hiyo ni mojawapo ya mikakati ya kuboresha mji wa Malindi ambao ni tegemeo kubwa katika sekta ya utalii ndani ya kaunti hiyo.

Kingi amesema lengo kuu la miradi hiyo ni kuimarisha uchukuzi kwa wakazi pamoja na usafirishaji wa mizigo , katika juhudi za kuboresha uchumi wa kaunti ya kilifi.

Kauli ya Gavana huyo inajiri siku chache tu  baada ya rais Uhuru Kenyatta kuzindua barabara ya Malindi-Salagete ambayo ni tegemeo kubwa kwa wadau wa utalii mjini Malindi.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Show More

Related Articles