HabariPilipili Fm

Wakaazi Wa Kilifi Watishia Kuwaua Wanyama Pori

Viongozi eneo la Magarini kaunti ya Kilifi wametishia kushawishi wananchi kuwauwa wanyama pori, ikiwemo Simba na Chui endapo serikali haitachukua hatua haraka iwezekanavyo.

Kulingana na viongozi hao,wanyama hao ambao wanarandaranda ovyo, wanatokea msitu wa Tsavo mashariki, kwa muda mrefu na sasa wamekuwa wakiwahangaisha wakaazi kwa kufanya uharibifu mkubwa wa mimea na mifugo, sawia na kuathiri maisha ya wenyeji.

Mbunge wa eneo hilo Harrison Kombe, wawakilishi wa wadi Renson Kambi wa Marafa, na Elina Mbaru wa Magarini wamedai kuwa maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori KWS, wamefeli kudhibiti mgogoro baina ya wakaazi na wanyamapori eneo hilo, licha ya wakazi kulalama kwa mda mrefu.

Hata hivyo kamishna wa kaunti ya Kilifi Joseph Keter amewasihi wakaazi eneo hilo kutochukua sheria mikononi mwao huku akiwataka walioathirika  kupiga ripoti kwa maafisa wa polisi akisema serikali inatafuta suluhu la kudumu.

Show More

Related Articles