HabariK24 TvSwahiliSwahili Videos

Chama kipya cha Jubilee Party kuzinduliwa rasmi

Mikakati ya uzinduzi wa chama kipya cha Jubilee inazidi kushika kasi Nairobi huku ratiba ya jinsi mtiririko wa mambo utakavyokuwa ikitarajiwa kutolewa kesho virasmi.

Wajumbe wapitao 10,000 kutoka vyama zaidi ya 13 vinavyotarajiwa kufunganya hadi Jubilee party wakitarajiwa kukutana katika ukumbi wa Bomas na wengine Kasarani kabla ya wao kuidhinisha chama Ijumaa 9 Septemba.

Rais Uhuru Kenyatta atahutubia siku ya Jumamosi 10 Septemba, wakati wa uzinduzi rasmi siku ambayo chama cha ODM kimepanga mkutano mkuu mombasa kwa mujibu wa gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho anayesema kuwa kutakuwa na tangazo kuu.

Show More

Related Articles