HabariMilele FmSwahili

Mututho amlaumu Kinuthia Mbugua kwa kulemaza vita dhidi ya pombe haramu Nakuru

Aliyekuwa mwenyekiti wa NACADA John Mututho amemlaumu gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua kwa kuhujumu juhudi za kupambana na biashara ya pombe haramu eneo hilo.Mututho amesema Nakuru bado ina visa vingi vya watu wanaofariki kutokana na athari za unywaji pombe haramu. Mututho amesema hatua ya gavana huyo kuzuia ukaguzi wa kila mara kwa maeneo ya burudani kunatoa mwanya kwa biashara hiyo haramu kuendelea.

Show More

Related Articles