HabariMilele FmSwahili

Wakili Patrick Onyango amefunguliwa mashitaka 15 kuhusiana na sakata ya NYS

Wakili wa mahakama kuu Patrick Onyango Ogolla amefunguliwa mashitaka 15 ya ulanguzi wa shilingi milioni 791 kuhusiana na sakata ya shirika la NYS. Akiwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya milimani Joyce Ghadhani Ogolla ameshitakiwa pamoja na mamake Ben Gethi Charity Wangui  baada ya kujaribu mara kadhaa kuzuia kushitakiwa. Wawili hao wamekanusha mashitaka na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu pesa taslimu au bondi ya milioni moja. Kesi yao itatajwa tarehe 22 mwezi huu.

Show More

Related Articles