HabariMilele FmSwahili

Mwanamume amejitia kitanzi baada ya mzozo wa nyumbani Malava

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 25 katika kijiji cha Cheroso eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega amejitia kitanzi kufuatia mzozo wa nyumbani. Kulingana na mkewe marehemu Simon Lumonje wawili hao waliuza kuku na fedha hizo zilinuia kukarabati nyumba yao japo mambo yakaenda mrama alipomuuliza marehemu kubaini kwa nini alienda kinyume na makubaliano yao. Tukio hilo limedhibitishwa na chifu wa kata ya Shianda Alfred Muhati.

Show More

Related Articles