HabariMilele FmSwahili

Ruto, Khalwale watofautiana hadharani kuhusu chama kipya cha Jubilee

Siasa za uchaguzi mkuu ujao zimetawala mkutano wa sherehe za kila mwaka za tamaduni ya jamii ya Butsotso, huko Kakamega, viongozi wa jamii ya magharibi wakitofautiana hadharani kuhusu mirengo ya kisiasa watakayofuata.

Naibu Rais William Ruto aliyekuwa katika hafla hiyo amekariri kuwa ni chama kipya cha Jublee pekee ambacho kitanusuru taifa kutoka kwenye siasa za kikabila, akiwataka wenye jikujiunga nacho.

Hata hivyo seneta wa Kakamega dkt Bony Khalwale alitumia hafla hiyo kuwaraia wenyeji kujitenga na siasa za Jubilee na kuwataka kuunga mkono muungano wa CORD.

Naye waziri wa maji Eugene Wamalwa ametilia mkazo wito wake kwa viongozi wamagharibi waliotangaza kuwania urais kubadili nia kujiunga na Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker