HabariSwahili

Tobiko Na Mwigai Wapewa Siku 14 Kujitayarisha Na Kesi.

Mkrugenzi  mkuu wa mashataka ya umaa Keriako Tobiko pamoja na  mkuu wa sheria Githu Mwigai wamepewa siku 14 kujitayarisha na Kesi ya kufungwa kwa akaunti za benki ya mashirika ya Muhuri na Haki Afrika.

Haya yanajiri  baada ya maafisa kutoka afisi hizo mbili kuomba muda zaidi wakujitayarisha kwa kesi hio.

Hata hivyo ombi la wawili hao limepingwa vikali na wakili wa shirika la kitaifa la utetezi wa haki za binadamu KNHCR, Victor Kamau ambaye ameyambia mahakama kuwa jambo hilo ni ukiukaji wa haki za binadamu na kuitaka mahakama kuharakisha kusikiliza kesi hyo ili haki ipatikane.

Akauti za benki za mashirika hayo zilifungwa na serikali baada ya kutuhumiwa kufadhili makundi ya kigaidi nchini.

Kesi hiyo itasikilizwa Oktoba 2 mwaka huu.

Show More

Related Articles