HabariSwahili

Ubaradhuli Wa Ubakaji.

Mtoto mmoja wa umri wa Miaka mitano anaendelea kuuguza majeraha ya ubakaji katika hospitali ya Jocham hapa Mjini Mombasa baada ya kubakwa na mpita njia na kujeruhiwa vibaya sehemu zake za siri.

Kulingana na mamake Mtoto huyo Irene Nekesa, mwanawe alikumbana na unyama huo mwendo wa saa tatu asubuhi siku ya jumapili wakati akielekea kwa mjombake eneo la Kisauni kabla ya kuokolewa na wapita njia waliompeleka hospitalini ili kupata matibabu zaidi.

Daktari mkuu wa maswala ya Uzazi,Emma Mwaura  amesema  mtoto huyo kwa jina Sarah Khabuya ambaye tayari amefanyiwa upasuaji wa kwanza, anahitaji upasuaji wa pili katika sehemu za siri shughuli ambayo huenda ikachukua muda wa miezi miwili kupona.

 

Show More

Related Articles