HabariPilipili FM NewsSwahili

Jeshi La KDF Laanzisha Oparesheni Kwenye Msitu Wa Boni.

Kundi la kwanza la vikosi vya usalama humu nchini limeweka kambi kadhaa katika mikoa mine ndani ya kaunti mbili zinazopakana na msitu wa boni, baada ya inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinet kutangaza eneo hilo kama eneo hatari.

Kikosi cha jeshi la Kenya KDF na kikosi maalum cha GSU pamoja na maafisa wa polisi, wameweka kambi katika maeneo Bodhai, na Hulugo huko Ijara kata ndogo ya kaunti ya Garisa, huku kundi jingine likiweka kambi maeneo ya Mangai na Baure kaunti ya Lamu.

Oparesheni hiyo ya miezi mitatu inatarajiwa kuwafurusha wanamgambo wa kundi la Alshabab ambao wameripotiwa kujificha ndani ya msitu wa boni ulio karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Inaarifiwa kuwa tayari jeshi la KDF limeanza kushambulia sehemu za msitu huo kwa kutumia ndege za Helicopters ambapo pia inadaiwa kuwa kuwasili kwa vikosi vya usalama eneo hilo kumesababisha hofu kwa wenyeji ambao wengi wao ni wakimbizi kutoka eneo la basuba kaunti ya Lamu.

Kati ya jamii ambazo zimetajwa kuathirika ni jamii za Wata na Wasanye ambao ni wawindaji na pia hujihusisha na shughuli za kilimo.

Show More

Related Articles