HabariPilipili FM NewsSwahili

KNUT Yataka Maafisa Wa TSC Kuchunguzwa Kwa Ufisadi.

Muungano wa kitaifa wa walimu KNUT kanda ya pwani sasa unataka maafisa wa tume ya kuajiri walimu TSC kuchunguzwa kwa madai ya kuhusika na ufisadi.

Wito huu unajiri huku walimu wakiendelea na mgomo kwa siku ya tano ambapo shughuli za masomo katika shule za umma zimeathirika pakubwa.

Walimu wapatao elfu moja wakiongozwa na katibu wa KNUT tawi la Kilindini Dan Aloo wamefanya maandamano kutoka katika afisi za KNUT zilizoko Changamwe hali ambayo imesababisha shughuli za uchukuzi katika eneo hilo kusimama kwa muda.

Aloo amesema TSC inazuia kimaksudi nyongeza yao ya mishahara na wakati umefika kwa maafisa wa tume hiyo kuchunguzwa.

Walimu hao wameishtumu TSC kwa kukiuka agizo la mahakama la kuamuru wapewe nyongeza ya mishahara na kwa sasa wametoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati swala hilo ili kuona kuwa wanapata haki.

Show More

Related Articles