HabariPilipili FM NewsSwahili

Ufisadi Waathiri Utoaji Wa Vitambulisho Humu Nchini.

Utafiti uliofanywa na Tume ya haki na utawala(afisi ya Ombudsman) umeonyesha kuwa ufisadi umeathiri pakubwa utoaji wa vitambulisho humu nchini ambapo mtu huhitajika kuwa na shilingi elfu 40 ili kuweza kupata cheti hicho.

Mwenyekiti wa tume hiyo Otiende Amollo amesema kukithiri kwa ufisadi kunachangia magaidi zaidi humu nchini, kwani kulingana na utafiti wakaazi kama vile wa Garissa huhitaji kutoa kitita cha shilingi elfu 45 kupata kitambulisho .

Utafiti huo vilevile umedhihirisha kuwa utoaji wa vitambulisho umekuwa wa kiubaguzi kwani siasa imeingizwa ndani yake, suala ambalo ni kinyume cha sheria.

Utafiti huo ulifanywa katika kaunti 17 humu nchini.

Show More

Related Articles