HabariPilipili FM NewsSwahili

Mfanyikazi Wa EPZ Apigwa Risasi na Polisi Mombasa.

Mfanyikazi mmoja wa kiwanda cha EPZ kilichoko Mazeras amefyatuliwa risasi na kuuawa mapema leo kufuatia makabiliano kati ya wafanyikazi wa kiwando hicho na maafisa wa polisi.

Inaarifiwa kwamba wafanyikazi wa kiwanda hicho walikua wakishiriki maandamano kupinga dhulma wanazotendewa na wasimamizi wa kampuni hiyo ambapo shughuli za usafiri kwenye barabara kuu ya Mombasa –Nairobi katika eneo la Mazeras zilitatizwa kufuatia maandamano hayo.

Duru za habari zinaarifu kwamba maafisa wa polisi walikua na wakati mgumu wa kutuliza wafanyikazi hao ambao walikua wakirusha mawe huku wakichoma matairi katikati ya barabara hiyo.

Kwa sasa inaarifiwa kwamba hali ya utulivu imeanza kurejea katika eneo hilo.

Show More

Related Articles