HabariMilele FmSwahili

Watu wanao tembea kando ya barabara ni waathirwa wakuu wa ajali

Watu ambao hutembea kando kando ya barabara ndio waathiriwa wakuu wa visa vya ajali za barabarani. Ripoti kutoka kwa mamlaka ya usalama barabarani inasema kati ya vifo 1,971 vinavyotokana na ajali hizo 845 ni vya watu ambao hutembea. Wamefariki kati ya kipindi cha utoka Januari hadi Agosti mwaka huu. Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa abiria 456 wamefariki kwenye visa hivyo sawa na madereva 222. Kamanda wa trafiki Charlton Muriithi anahusisha idadi kubwa ya vifo vya wanaotumia barabara kwa miguu na tabia zinazohatarisha maisha yao.

Show More

Related Articles