HabariMilele FmSwahili

57% ya wakenya waunga mkono kuwepo kwa majeshi ya Kenya Somalia

Asilimia 57 ya wakenya wanaunga mkono kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la IPSOS Synovate, miongoni mwa waliounga mkono swala hilo asilimia 70 ni wafuasi wa Jubilee huku 39 wakiwa wafuasi wa CORD.Aidha eneo la kati linaongoza kwa wanaounga mkono swala hilo kwa asilimia 80 ikifuatwa na Rift Valley kwa asilimia 62.Ripoti hiyo pia imeonyesha kupungua kwa visa vya uhalifu nchini japo Nairobi bado inaongoza kwa asilimia 14, eneo la kaskazini mashariki kwa asilimia 10 na Rift Valley asilimia 39.Utafiti huo ulifanywa miezi mitatu iliyopita na kuwahusisha wakenya 2002.

Show More

Related Articles