HabariMilele FmSwahili

KNUT yawasilisha kesi mahakamani dhidi ya TSC

Chama cha walimu nchini KNUT kimewasilisha kesi mahakamani dhidi ya tume ya kuwajiri waalimu kwa kukiuka agizo la mahakama.KNUT inadai TSC inapaswa kuchukuliwa hatua kwa kukiuka agizo la kuwapa walimu nyongeza ya asilimia 50 hadi 60 ya mishahara yao.Kesi hiyo imeorodheshwa kama ya dharura na itasikizwa na jaji Nduma Nderi. Mudzo Nzili ni mwenyekiti wa KNUT
Kando na hayo Nzili ameikosoa tume ya kuwaajari walimu kwa kutishia kuwafuta kazi waalimu wanaogoma. Katika mahojiano na milele fm Nzili anadai waalimu watasalia nje ya madarasi hadi pale watakapokabidhiwa nyongeza hiyo.
Wakati huo huo baraza la kitaifa la mitihani limeelezea matumaini ya kutatuliwa mgogoro wa mishahara ya waalimu hivi karibuni.Afisa mkuu mtendaji wa KNEC Joseph Kivilu anasema wameweka mikakati itakayohakikisha wanafunzi wa kidato cha nne na wale wa darsa la nane katika shule za umma hawaathiriki.

Show More

Related Articles