HabariPilipili FM NewsSwahili

Wahudumu Wa Fuo za Bahari Kupata Mafunzo Kaunti Ya Kwale.

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amezindua mradi wa mafunzo ya kwanza kabisa kwa wahudumu wa fuo za bahari katika eneo hilo.

Akiongea baada ya kuzindua rasmi mafunzo hayo ya wiki sita katika kituo cha biashara cha Kwale,Mvurya amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapa wahudumu hao ujuzi wanaohitaji kutekeleza majukumu yao.

Mvurya aidha amesema kwamba wamehusisha washikadau wote , hio ikiwa njia mojawapo ya kumaliza dhulma wanazopitia wahudumu wa fuo za bahari kutekeleza majukumu yao.

Wakati huo huo naibu gavana wa kaunti hiyo Fatuma Achani amesema serikali ya kaunti hiyo imeanzisha harakati ya kutengeneza barabara zinazoelekea katika fuo za bahari pamoja na kujenga maduka kwa wahudumu hao.

Show More

Related Articles