HabariPilipili FM NewsSwahili

Mwanamke Akamatwa Na Bhangi Malindi.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 36 amekamatwa akiwa na bhangi yenye thamani ya shilingi elfu 40 na maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria katika eneo la Mtangani wilayani Malindi.

Akithibitisha kisa hicho afisa mkuu wa polisi wilayani humo Matawa Muchangi amesema Fatuma Kiponda Gandi amekamatwa na bhangi hiyo yenye uzani wa takriban kilo 4.8 ndani ya mtungi mweusi.

Wakati huo huo takriban shilingi laki 3 noti za shillingi 50 na 100 zinazodaiwa kuwa mapato ya dawa za kulevya zimepatikana juu ya dari kwenye nyumba ya mwanamke mmoja eneo la Kisumu Ndogo wilayani humo.

Wawili hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Malindi pindi uchunguzi utakapokamilika.

Show More

Related Articles