HabariMilele FmSwahili

Mtoto atoweka kwa njia isiyoeleweka katika hospitali kuu Machakos

Kumetokea kizaa zaa katika hospitali kuu ya Machakos baada ya kutoweka kwa njia isiyoeleweka kwa mtoto mchanga aliyezaliwa hospitalini humo na mwanamke mmoja kwa jina Mary Njeri Wanyoike kwa mujibu wa bwanake Benard Muoki ni kwamba Njeri alimuonyesha mwanawe kwa kumpiga picha huku akipewa mtoto mwingine tofauti baadaye ambaye alifariki saa chache. Juhudi za kumfikia afisa mkuu wa kitengo cha afya katika serikali ya kaunti ya Machakos zimegonga mwamba.

Show More

Related Articles