HabariPilipili FM NewsSwahili

Serikali Yaifanyia Mabadiliko Sekta Ya Usalama Nchini.

Serikali imetangaza mabadiliko makubwa katika sekta za usalama na utawala katika azimio la kukabiliana na tatizo la ugaidi, wizi wa mifugo, unywaji wa pombe haramau pamoja na ulanguzi wa mihadarati humu nchini.

Mabadiliko hayo yameathiri makamishna 33 wa kaunti pamoja na makamanda wakuu wa polisi ambao wamelazimika kupewa uhamisho.

Maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko hayo ni kaunti ya Nairobi, Mombasa, Kisumu pamoja na kaunti zote za kaskazini mwa Kenya ambapo usalama umesalia kuwa tishio kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab.

Waziri wa usalama wa nchi Joseph Nkaissery amesema mabadiliko hayo mapya yataanza kutekelezwa maramoja huku akiwaamuru maafisa wote walioathiriwa kufika katika vituo vyao vipya kabla ya jumatatu wiki ijayo.

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amesalia kwenye wadhfa huo huku Francis Wanjohi akichukuwa nafasi ya Robert Kitur.

Mabadiliko hayo yanajiri siku moja baada ya rais Uhuru Kenyatta kumteua Joel Kitili kuwa naibu inspekta generali wa polisi.

Show More

Related Articles