HabariMilele FmSwahili

Nkaiserry afanya mabadaliko katika idara ya polisi

Idara ya polisi imefanya mabadiliko machache ya makanda wake na makamishna wa kaunti. Akitangaza mabadiliko hayo, waziri wa masuala ya ndani Joseph Nkaiserry anasema yanapania kupambana na wizi wa mifugo, vita dhidi ya mihadarati na pombe haramu sawa na kudumisha usalama kote nchini. Miongoni mwa maafisa waliopewa uhamisho ni kamishna wa Nairobi Njoroge Ndirang’u na Kamanda Benson Kibue. Kamishan wa kaunti ya Mandera Alex Nkoyo amehAmishiwa Kiambu, kamihsna wa kaunti ya Baringo Peter Okwany naye amehamishiwa Tana River. Nelson Marwa atasalia kaunti ya Mombasa.

Show More

Related Articles