HabariMilele FmSwahili

Kanisa katoliki laghadhabishwa na mgomo wa walimu

Kanisa katoliki limeonyesha kughadhabishwa kwake na mgomo wa walimu unaoendelea na kutoa wito kwa washikadau husika katika sekta ya elimu pamoja na wizara ya fedha kuafikia mwafaka. Wameshikilia kuwa amri ya mahakama lazima iheshimiwe hata hivyo kuwataka walimu kuipa muda serikali kutekeleza hilo. Mwenyekiti wa kamati inayosimamia maswala ya elimu katika miungano ya maaskofu wa kanisa katoliki Rev Maurice Makumba ametaka mwafaka kuafikiwa kuwanusuru wanafunzi wanaojiandaa kwa mitihani ya kitaifa.

Show More

Related Articles