HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya watu elfu mia tatu wanaathirika na njaa Turkana

Wabunge saba kutoka eneo la Turkana na seneta John Munyes wametoa tahadhari dhidi ya baa la njaa linalowaathiri wenyeji wa Turakana zaidi ya elfu mia tatu. Katika ziara ya siku tano ya viongozi hao ya kusambaza msaada wa chakula na maji katika eneo hilo imebainika kuwa ukame unaosababishwa na ukosefu wa mvua umewaathiri wenyeji wengi. Wenyeji hao wanalalamikia fedha nyingi zinazorejeshwa katika wizara ya fedha mwishoni mwa mwaka wa kifedha huku hali yao ikiendelea kuathirika.

Show More

Related Articles