HabariMilele FmSwahili

Waendesha mashtaka 2 wakamatwa kwa dai la kupokea hongo

Waendesha mashtaka wawili wamekamatwa na maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi kwa dai la kupokea hongo ya shilingi elfu 15 ili kufungua tena faili iliyokuwa imeamrishwa kufungwa na maafisa wa polisi.Herbert Okumu na Kipyegon Ruto wanaohudumu katika afisi ya mwendesha mashtaka mkuu Kisumu walikamatwa wakiomba hongo kutoka kwa Henry Ongwetto kufungua tena faili hiyo.Wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 20,000 na wanatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya EACC kaunti ya Homabay jumatano wiki ijayo.

Show More

Related Articles