HabariSwahili

LSK Yasema Mutua Aache Kutumiwa Na Mutunga.

Chama cha mawakili( LSK) kanda ya pwani kimemtaka mwenyekiti wao mkuu Erick Mutua kuacha kutumiwa vibaya na jaji mkuu willy mutunga.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa LSK tawi la Mombasa ,Erick Nyongesa ambaye pia ndiye mwenyekiti wa chama hicho Mombasa amesema tangu waanze mchakato wa kutaka kumuondoa mamlakani jaji mkuu ,Mutua amekua kimia huku akisema hajapata rasmi malalamishi ya wanachama kutoka Mombasa na kanda ya pwani kuhusiana na maombi yao yakutaka kuondolewa mamlakani kwa jaji mkuu.

Nyongesa amesema Mutua ambaye ndiye mwenyekiti wa LSK anatumiwa vibaya na anafinyiliwa ili asikiri ubathirifu unaondelezwa na jaji mkuu hivyo wakamtaka ajitokeze kimasomaso ili aseme msimamo wake.

Wakati huohuo Nyongesa amesema  tayari wamewasilisha maombi yao kwenye kamati ya bunge ianayohusiana na haki  na maswala ya kikatiba wakitaka Willy Mutunga ang’olewe mamlakani kwa kile wanachokitaja kushindwa kutekeleza majukumu yake kikatiba,ubathirifu wa fedha na utumizi mbaya wa afisi.

Awali chama hicho kiliandaa ukusanyaji wa saini elfu moja kutoka kwa wadao wa sharia na wananchi ili kusukuma maazimio yao na pia katika kongamano la kitaifa la kila mwaka la mawakili lilofanyika kusini mwa pwani swala hilo liliangaziwa huku baadhi ya mawakili wakiunga mkono dhamira ya Nyongesa.

 

Show More

Related Articles