HabariMichezoMilele FmSwahili

Ruto awalaki wanariadha wakenya walioibuka mabingwa Beijing

Naibu rais William Ruto amewapongeza wanariadha wa Kenya waliowasili nchini mapema leo baada ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya riadha yalokamilika juma hili huko beijing china. Akielezea furaha yake kuhusu jitihada za wanariadha hao, Ruto ameahidi serikali ya Jubilee itaboresha na kutoa nafasi kwa vijana kupitia michezo,huku kikosi cha Kenya kikitarajia kukutana na Rais Uhuru Kenyatta alhamisi hii.

Nahodha wa kikosi cha Kenya Ezekiel Kemboi amedokeza huenda akastaafu baada ya kutawala dunia huku mashindano ya Olimpiki yakiwa yake ya mwisho kama nyota wa taifa.
Kenya ilimaliza katika nafasi ya kwanza duniani kwa kujizolea nishani 16,7 za dhahabu sita za fedha na tatu za shaba.

Show More

Related Articles