MichezoMilele FmSwahili

Manchester United kumsajili Anthony Martial

Klabu ya Manchester United iko katika hatua za mwisho za kumsajili mshambulizi matata wa klabu ya Monaco ya Ufaransa Anthony Martial mwenye umri wa miaka 19. Haya yote yamejiri wakati manchester united wamepigwa mabao 2-1 na Swansea City hapo jana huku wataalamu wakidadisi kuwa Wayne Rooney anahitaji mshambulizi wakumsaidia kutafuta magoli.
Msimu huu Wayne Rooney hajapachika boa lolote wavuni akichezea Manchester United katika ligi kuu ya uingereza.
Van Gaal anasema Anthony Martial atasaidia pakubwa kwenye safu ya ushambulizi ya manchester united baada ya kupoteza tumaini la kumchukua mshambulizi wa Barcelona Neymar ama Gareth Bale wa Real Madrid
Klabu ya Manchester United inamtaka mfaransa huyo anayechezea klabu ya Monaco kwa kimo cha paunti €50m (£36m)
Gazeti la Le Parisien la ufaransa limesimulia kuwa Martial ashaafikiana na mashetani wekundu na huenda akapewa kandarasi ya miaka kadhaa huko Old Trafford.
Anthony Martial amesafiri hii leo klubu ya manchester United kwa uchunguzi wa kiafya

Show More

Related Articles